Advertisements

Tuesday, February 21, 2017

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aachiwa na polisi usiku wa kuamkia leo.

Hatimaye Jeshi la Polisi nchini limemwachia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe baada ya kumshikilia kwa saa 10. Ofisa Habari wa chama hicho Tumaini Makene, amethibitisha kuachiwa kwa Mwenyekiti huyo ambapo pia amesema polisi wamemtaka kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kesho Jumatano.  
Mbowe aliachiwa saa saba usiku wa kuamkia leo baada ya kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake na kukutwa ambako polisi hawakukuta dawa za kulevya zaidi ya nyaraka mbalimbali za chama zikiwamo Hati moja ya Chadema-Chaso kwenda kwa Mwenyekiti ya Julai 16, mwaka 2013, picha mbalimbali nane za matukio ya uhalifu, hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya Chadema kuhusu uundwaji wa Red Brigade na hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano. 
 Hata hivyo, pamoja na Mbowe kuachiwa na polisi Makene amesisitiza kwamba kesi yake aliyomfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya iko pale pale.

No comments: