Serikali imetoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa wizara ya Elimu ikiwa kuna chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya, mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililohusu kwamba kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania.
Mhandisi Manyanya alijibu, “Sarafu inayotakiwa kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania malipo ya kitu au
huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua.
huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua.
Aliongeza “Japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo Septemba 07, 2016. Vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania. Natoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa wizara ya Elimu ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.”
Mkutano wa Bunge uliopita swali kama hili liliwahi kuulizwa, na bado serikali imeweka mkazo kukataa wanafunzi wa kitanzania kulipa ada kwa fedha hizo.
No comments:
Post a Comment