ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 9, 2017

Shinda Nyumba Droo ya Kwanza Yafanyika kwa Kishindo

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Global Publishers, Soud Kivea (kulia) akikabidhi zawadi ya fulana kwa mshindi.
Mr. Shinda Nyumba akichanganya rundo la kuponi wakati wa Droo ya Kwanza ya Shinda Nyumba, iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala, Zakhem.
Msomaji akichanganya kuponi wakati wa droo hiyo.
Msomaji akiwa amefungwa nguo ngumu machoni akitafuta kuponi kwenye rundo la kuponi ili kumpata mshindi wa droo hiyo.

Mshereheshaji, Mc. Chaku akisoma jina la mshindi.




Jina la mshindi likisomwa.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemmed (kushoto) akiandika majina ya washindi wa Droo ya Kwanza ya Shinda Nyumba, katikati ni Soud Kivea na kulia Elvan Stambuli (wote ni wawakilishi wa Global Publishers).

Orodha ya majina ya washindi wa Dropo ya Kwanza ya Shinda Nyumba.

Na Mwandishi Wetu | Global Publishers DROO ya kwanza ya Shindano la Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili imefanyika leo Feb 8, 2017 kwa kishindo katika Viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar ambapo tayari wamepatikana washindi wa zawadi za pikipiki, televisheni, simu za kisasa na vyombo vya nyumbani. Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho amesema kuwa, droo hiyo iliyofanyika ni ishara tosha ya kuanza rasmi kwa droo nyingi ndogondogo zitakazofanyika pia hadi mikoani, kuelekea droo kubwa ambayo itamtoa mshindi wa nyumba ya mamilioni ya shilingi iliyojengwa Dar. Washindi waliopatikana katika droo hiyo ya kwanza ni Andrew Mtunguja wa Muheza Tanga (Pikipiki), Amarosi Mgonja wa Mangula (TV), Evansi Stanley John wa Kunduchi Dar (Smartphone), Gasto Peter wa Kimara (Dinnerset) na Said Mohammed wa Kimara jijini Dar ( Smartphone). Akiendelea kuzungumzia shindano hilo, Mrisho aliwataka wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Championi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda kuendelea kusoma zaidi na kujaza kuponi ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi. “Kuponi zote zitakazopokelewa zitashiriki katika droo zote, hata zile zitakazochezwa mikoani, kwa hiyo mtu anakuwa katika nafasi nzuri ya kupata ushindi endapo atakuwa na kuponi nyingi, ingawa siku zote bahati ni bahati tu, mshindi anaweza kushinda hata kwa kujaza kuponi moja tu,” alisema Mrisho. Shinda Nyumba awamu ya pili inadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) yenye vituo vyake katika maeneo mengi nchini ikiwemo Bamaga, Tabata Kimanga, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mkuranga, Muheza, Vigwaza, Songea na Lindi.

No comments: