ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 7, 2017

Spika akataa Trump kuhutubia bunge Uingereza-BBC

Spika wa bunge la Uingereza John Bercow
Spika wa Bunge la Uingereza John Boscow amekosolewa kwa kupinga hatua ya rais Donald Trump kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake.

Mwanachama wa chama cha kihafidhina aliambia BBC kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja.

Bw Bercow alisema pingamizi dhidi ya ''ubaguzi wa rangi na ule wa kijinsia'' zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge hilo.

Mbunge wa Marekani Joe Wilson alisema kuwa ni pigo kwa chama cha Trump cha Republican.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa Eleanor Garnier amesema kuwa ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo.

Mwezi uliopita waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alisema kuwa rais Trump amekubali mwaliko kutoka kwa malkia wa Uingereza kwa ziara rasmi nchini Uingereza baadaye mwaka huu.

Lakini akizungumza bungeni siku ya Jumatatu bw Bercow alisema kuwa anapinga rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo ada na viongozi wengine wa kimataifa.

Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa.

'Nahisi kwamba pingamizi yetu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na ue wa rangi na haua yetu ya kuunga mkono usawa na uhuru wa mahakama ni muhimu sana na yanapaswa kupewa kipaumbele na wabunge wa Uingereza'', alisema.

No comments: