Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya.
Aidha amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituo cha polisi kesho.
Akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii, RC Makonda amewataka wauzaji wote kufika makao makuu ya polisi kwajili ya kujieleza.
“Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,” alisema Makonda.
Aliongeza,’Wapo tuliowakamata pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo yanayotakiwa. Lakini wapo ambao bado, majina ni mengi sana mtayapitia wenyewe, kuna Mchafu, Director Joan, Mirror, Rommy na wengine wengi, wapo wauzaji wadogo na wengine wakubwa. Lakini wapo wengine wanasemekana wanatumia lakini hakuna ushahidi kwamba wanatumia ingiwa wenzao wanasema wanatumia, ni bora nikakutana nao kesho pale Central, akiwemo TID, Wema Sepetu,”
List ya watuhumiwa
RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi
Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata - RC Makonda
Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe - RC Makonda
Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari - RC Makonda
Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya - RC Makonda
3 comments:
Waandishi wana blog mmetuletea habari na mawazo ya wadau myachapishe pia ili kujifunza! Sawa unaweza ukawa sahihi kwa uliowataja. Ila tu kwa ufahamu wa walio na kumbukumbu. Hao ni vidagaa vilivyochoka! Ungewasiliana na yule unayempigia simu kutafuta kiki anayo majina ya yale mapapa yanayoingiza na kusambaza hiyo miunga! Orodha iliyoachwa na watangulizi.ilishindikana kutumbua itakuwa hii!.
Vipi walioanikwa shisha wameishia wapi na kupiga hodi kwa wadada poa!
Tuwe wa kweli kwa mambo.mengi yanaibuliwa na kuishia hewani na hii ndio Tanzania tuu mambo haya yapo kwa viongozi wetu! Tatizo kubwa ni viongozi wa kuteuliwa na kuapishwa bila kupitishwa na wabunge au jopo la mawaziri! Unateuliwa kizani unaapishwa juani!!
Waalimu.kusafiri bure Dar inaendelea au ndio maana tumepasisha sana wanafunzi wa kidato 4.
Yeeeees ,safi sana mzee makonda, kazi nzuri sana,tunaomba uwataje na maboss wenyewe,
Ni ujasiri wa hali ya juu kwa upande wa Makonda na anastahili pongezi kwa uthubutu lakini kwa approach hii ya kuja public na majina ya waathirika na pengine street pushers nadhani jitihada hizi zitaishia hapox2.pengine mwisho wa siku kusiwe na effect yoyote kwakuwa wote waliotajwa wako way too low kwenye food chain.
Post a Comment