Saturday, February 11, 2017

Wahamiaji wasio na vibali wakamatwa Marekani-BBC

Wahamiaji
Watetezi wa haki za wageni, wanasema mamia ya wahamiaji wasiokuwa na nyaraka za kubaki Marekani, wamekamatwa nchini humo katika siku chache zilizopita.

Wanasema kuwa maafisa wa uhamiaji walifanya misako Los Angeles, Atlanta, Chicago, New York, Texas na Carolina Kaskazini, katika hatua za kufuata sheria chini ya serikali mpya ya Rais Trump.

Lakini wakuu wanasema misako hiyo ni ya kawaida, ya kuwakamata wahamiaji wahalifu na kuwaondosha nchini.

Wanasema hatua kama hizo zilikuwa zikifanywa wakati wa serikali zilizopita

Shirika la kutetea haki za wahamiaji la Los Angeles, limesema mahabusu hawaruhusiwi kuwaona mawakili.

Hapo awali, serikali ya Mexico, ilionya raia wake walioko Marekani, wawe na tahadhari, na wawasiliane na ubalozi wao, baada ya mwanamke mmoja kutoka Mexico kuondoshwa kwa lazima siku ya Alkhamisi.

No comments: