Serikali ya DRC imeahidi kuruhusu jeneza lake kupelekwa bungeni na pia kusema kuwa itawalipia ndege waliokuwa wanasiasa wenzake hadi Ubelgiji kuuchukua mwili huo.
Hata hivyo, chama cha Tshisekedi cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), kimekataa pendekezo hilo na badala yake kutangaza masharti yake.
Chama hicho kilisema serikali inastahili kumjengea makumbusho Tshisekedi katikati ya mji wa Kinshasa na pia kimetaka gharama ya mazishi kulipwa na serikali inayokuja ambayo muundo wake umeafikiwa, ingawa bado haijaingia madarakani.
Maafikiano ya kubuniwa serikali mpya inayojumuisha muungano wa upinzani uliobuniwa na Tshisekedi ilikuwa na sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana.
Serikali imejibu masharti ya UDPS ya kujengwa kwa makumbusho, lakini imesema kuwa haitajengwa katikati ya mji.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment