Wananchi mkoani katavi wameiomba serikali kumuondoa meneja wa shirika la umeme Tanzanaia Tanesco mkoani humo kutokana na kushindwa kusimamia vizuri suala la upatikianaji wa umeme wa uhakika hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo yao.
Wakizungumza na Gazeti baadhi ya wananchi na wafanyabiashara walisema meneja wa shirika hilo mkoani hapa anapaswa kuondolewa kutokana na kushindwa kusimamia vizuri uapatikanaji wa nishati ya umeme hali ambayo imepelekea kupata hasara kubwa kutokana na kutokuwepo kwa umeme wa uhakika kwa muda wa wiki mbili sasa.
Walisema kuwa mpaka sasa wanashindwa kujua tatizo ambalo linapelekea kukosekana kwa umeme wa uhakika mkoani hapa huku baadhi ya bidhaa zao zikiendelea kuoza kutokana na kutegemea nishati hiyo hali ambayo inapelekea kurudi nyuma kimaendeleo.
Waliongeza kuwa wamekuwa wakipata majibu yasiyoridhisha kutoka kwa meneja wa Tanesco mkoni hapa pindi wanapohoji juu ya suala la kukatika kwa umeme mara kwa mara bila Taarifa na kusabaisha kuunguza vifaaa vyao majumbani na viwandani.
Aidha wananchi hao walisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inapaswa kutoa majibu ya uhakika juu ya upatikanaji wa nishati ya umeme mkoa ni hapa ili waweze kuondokana na changamoto hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma maendeleo yao.
Hata hivyo wananchi hao waliomba serikali kupitia kwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na waziri wa nishati na madini Profesa Sospiter muhongo kuutazama mkoa wa katavi katika suala zima la upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika ili kuondokana na changamoto hiyo.
Kwa upande wake meneja wa Tanesco mkonia hapa amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la umeme na kusema kuwa hali hiyo inasabishwa na uchakavu wa mitambo inayozalisha nishati ya umeme huku akiwatoa hofu wananchi kuwa tatizo hilo litakwisha muda si mrefu.
No comments:
Post a Comment