Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya(kushoto), alipofika ofisini kwake kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya(kushoto), akizungumza na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alipofika ofisini kwa waziri kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) ,baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka wizarani hapo, Harrison Mseke.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment