Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu
Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.
"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu
Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM na kusema "Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki
Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"
Msikilize hapo chini akiongea
4 comments:
Nonsense, kama unajihusisha na madawa unataka uwe exempted kwa sababu wewe ni Wema or you carry the Sepetu name? Does Chadema condone your behaviour? Is Chadema a refuge for Drug addicts and pushers? Drugs and Democracy are two different things, and please don't MIX the TWO D's. Give me a break, Nobody is above the Law PERIOD. Frankly, for CCM-a party with millions of members, the loss of a Mother and Daughter has no effect. WEMA SEPETU, you are no Royalty!!!
Hajui anachokitaka,anatapatapa tu,njaa tu hamna lolote
pamoja wema wataisoma number sasa.people's power. what a shame mtu unanyimwa ngono unalipiza kisasa.karibu sana wema chadema.people's power.
Major issue ni kuwepo kwa ukandamizaji qa aina fulani nchini Tz hasa kwa wapinzani na ukandamizaji huo umetengeneza a shell of fear na nidhamu ya woga.
Yes, kutakuwa na impact kisiasa kwa wema kuhamia Chadema, na magnitude ya hiyo impact is time that will tell.
Mtoa maoni hapo juu nadhani hajazingatia kwa makini on what actually going on in Tz.
With regard na tuhuma za mihadharati, no need to sweat now, wema is taken to court and we will see if she can be found guilty or not.
Hakuna haja ya kumuhukumu kwa kuwa by the law, you are innocent until proven guilty beyond reasonable doubts.
Post a Comment