Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza na Wanahabari
kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara
ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa wa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM
International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya
kuhakiki madai hayo.
Katika
Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi
cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi
wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya
kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya
kwanza ya Ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment