Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusua mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya 'NAMTHAMINI',Basilisa amebainisha kuwa kupitia EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za
Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na
pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673
kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.Pichani kulia ni Mratibu wa Vipindi Eastafrika Radio,Irene Tillya na kushoto ni Mratibu wa Vipindi EATV,Sophie Proches.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo kuhusiana na mafanikio makubwa waliyoyapata kupitia kampeni hiyo ya 'NAMTHAMINI',Kiria emesema kuwa Katika kampeni hiyo ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.
Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akifafanua zaidi mbele
ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na mafanikio ya
kampeni hiyo 'Namthamini',iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za
Kike) kwa wanafunzi wa Sekondari,ambapo takwimu zinaeleza kuwa karibia
asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi
kutokana na kukosa pedi za kujistiri.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mapema leo jijini Dar.
Kituo namba moja kwa vijana East Africa Television (EATV)
Limited kikishirikiana na Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA foundation)
kinapenda kutoa shukrani za dhati, kwa umma wa watanzania kwa
kufanikisha kuchangia kwenye kampeni ya Namthamini.
Namthamini ni kampeni
iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa wanafunzi wa Sekondari, kutokana na takwimu kuonesha
karibia asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi
kutokana na kukosa pedi za kujistiri.
Kwa wastani wanafunzi wa kike wengi hupoteza siku tano hadi
saba kila mwezi kutokana na ukosefu wa pedi za kujisitiri, na kwa mwaka
inakadiriwa kukosa masomo kwa takribani siku 60 hadi 70.
EATV na East Africa Radio katika kufikisha mchango wake kwa
jamii, na kwa kuangalia Siku ya Wanawake Duniani, Machi mosi tuliamua kuanzisha
kampeni hii kwa kuishirikisha jamii ili kumuwezesha mwanafunzi wa kike asikose
masomo yake na kumfanya kutofikia lengo lake kimasomo kwa kukosa pedi pale
awapo kwenye hedhi.
EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za
Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na
pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673
kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.
Katika kampeni hii ambayo wananchi walijitokeza kuichangia
katika kuonyesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya
shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani
ya shilingi 8,401,500.
Michango yote ya fedha iliyopatikana itatumika katika kununua
pedi na zitaelekezwa moja kwa moja katika shule za Sekondari 20 zenye uhitaji
zilizoteuliwa kupata msaada huu, katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Lindi, Pwani
na Tanga.
Uongozi wa EATV Limited na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa
Foundation) inapenda kutumia nafasi hii kwa dhati kuwashukuru wananchi wote
walioguswa na tatizo la pedi kwa wanafunzi wa kike na kuichangia kampeni ya
Namthamini na kuonyesha kuwa kwa pamoja tunaweza. Sisi EATV husema Together Tunawakilisha.
Mwisho kabisa tunapenda kusisitiza kuwa tatizo la wanafunzi
wa kike kukosa kuhudhuria shuleni kutokana na kukosa pedi za kujisitiri ni la
kwetu sote hivyo East Africa Television Limited pamoja na Taasisi ya Haki za
wanawake inatoa wito kwa jamii kuendelea kuungana kwa pamoja katika kusaidia
watoto wa kike kupata mahitaji muhimu wawapo shuleni, ili wapate kusoma kwa
amani pasipo kukosa kuhudhuria darasani.
No comments:
Post a Comment