Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo (katikati) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. (PICHA NA DALILA SHARIF)
Na Dalila Sharif
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amekagua ujenzi wa Daraja
linalounganisha Kijichi hadi Toangoma wilayani Temeke.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, alipokuwa
akikagua ujenzi wa daraja hilo, Naibu Waziri alisema ameridhishwa na maandalizi
ya ujenzi wa daraja hilo
“Daraja hilo lenye urefu wa mita 600 na inatakiwa matayarisho
yaanze mapema kwa kuchonga barabara ili
ujenzi ukamilike mapema tayari kwa wananchi kulitumia,”alisema Jafo.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Felix Lyaniva alisema anampongeza Naibu
Waziri kwa kukagua ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa ni nia njema katika
kuendeleza maendeleo ya wilaya hiyo.
Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu
alimuomba waziri kuwatatulia wananchi wa
eneo hilo kero inayowakabili ya kutolipwa
fidia zao.
“Wakazi wa eneo ambao hadi sasa hawajalipwa fidia ya
nyumba zao wamekuwa wakikumbwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua hivyo
kuathirika kwa kiasi kikubwa,”alisema Mangungu.
Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu maendeleo ya mradi huo
Jaffo akiwasili kukagua mradi huo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. (PICHA NA DALILA SHARIF)
Jaffo akitoa maagizo baada ya kukagua mradi huo
No comments:
Post a Comment