Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo (Ijumaa) imemuachia, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) kwa dhamana ya bondi ya Sh10 milioni.
Lissu amedhaminiwa na maelezo ya awali yatasomwa Aprili 3, mwaka huu.
Leo asubuhi, Lissu alisomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi likiwamo ya kutoa maneno yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.
Lissu ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.
No comments:
Post a Comment