
Aprili 29, 2016, Mstahiki Meya wa jiji la Dallas, jimbo la Texas aliitangaza rasmi siku hiyo kuwa SIKU YA TANZANIA
Na mwaka huu, Jumuiya ya waTanzania waishio jimboni humo kwa kushirikiana na Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America) wanaandaa maadhimisho makubwa ya siku hiyo yatakayofanyika katika jiji la Dallas.
Viongozi Ben Kazora wa Jumuiya ya Dallas na Charles Bishota wa DICOTA wamezungumza na Mubelwa Bandio kuhusu maandalizi ya siku hiyo
KARIBU USIKILIZE
2 comments:
mnaweza kufanikisha hiyo cku, kwa kila mmoja wenu akusanye ngoma mbali mbali za makabila yenu, vile vile kukusanya vinyago mbalimbali vya kuonyesha utu wa mtanzania na asili yake.
kuweka vyakula mbali mbali vya kitanzania kama ugali wa muhogo, mtama, ndizi mboga mboga za majani kama vile msusa, majani ya kunde, matembele, bamia,chainis, spinach, mihogo, magimbi, etc
by mbonde kizito from tanzania
Asante kwa ushauri kaka Kizito Mbonde.
Oliva
Post a Comment