Alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Godwin Ikema mbele Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa, Pascal Mayumba.
Upande wa mashitaka ulidai mahakamani kuwa mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili la kujeruhi, kumchoma moto mtoto wa miaka mitano kinyume cha Kifungu cha Sheria namba 225 ya Kanuni ya Adhabu Namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Kosa la pili ni kumfanyia ukatili mjukuu wake huyo (jina tunalo) kinyume cha Kifungu cha sheria namba 169 (a) kifungu E (1) na (2) cha kanuni na adhabu na 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 19, mwaka huu katika kijiji cha Rudi wilayani Mpwapwa na Mkoa wa Dodoma saa tano usiku.
Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na mahakama ilisema dhamana ya mshitakiwa iko wazi kama atatimiza vigezo na masharti ya dhamana ikiwa ni wadhamini wawili na kusaini dhamana ya maandishi ya Sh 500,000.
Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi hadi Aprili 6, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment