Madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo la mererani pekee duniani yakiwa tayari yamekatwa na kusanifiwa sasa yatauzwa kimataifa katika kituo kitakachonjengwa Arusha
Mtaalamu wa kukata madini Adam Idd Lacha akiwa anakata na kusanifu madini ya Tanzanite ya kampuni ya Tanzanite one ambayo ndio inatoa mafunzo hayo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa anapewa maelezo juu ya madini ya Tanzanite , na wakurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Juma na Hussein Gonga. Alipokuwa katika kituo cha kuuza madini cha kampuni hiyo.
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sky Associate Group, Faisal Juma Shahbhai akizungumza na madali wanawake wa madini
Muonekano wa Mgodi wa kisasa wa uchimbaji madini wa tanzanite One Mererani kwa nje
PICHA ZOTE NA MUSSA JUMA
ANDREA NGOBOLE, PMT
Kampuni ya Tanzanite One, imetoa msaada wa Sh 20 milioni kwa chama cha Madalali wanawake,wanaouza madini ya Tanzanite mkoani Arusha .
Wakurugenzi wa kampuni hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO), Faisal Shabhai na Hussein Gonga walitangaza uamuzi huo wakati wakizungumza na madalali , katika ukumbi wa polisi jijini hapa.
Faisal alisema kampuni yao ambayo inachimba Tanzanite, imetoa msaada wa sh 20 milioni,ili kuendelea kutekeleza mahusiano mema na wadau wa Tanzanite na jamii ya wanawake ambao wanajihusisha na biashara ya kuuza madini hayo.
Alisema msaada huo, umetokana na maombi ya wanawake hao, kusaidiwa waliyotoa katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na viongozi wa Tanzanite One.
Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetenga kiasi cha sh 200 milioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya kisasa Mererani.
Gonga alisema kwa sasa tayari wametoa matofali 65,000 ambayo yapo eneo ambalo itajengwa hospitali hiyo ili kuondoa matatizo ya ukosefu huduma za afya katika mji wa Mererani.
Awali Mwenyekiti wa chama hicho, Eugen Augustine alisema madalali wa madini wanawake mkoani Arusha, wanakabiliwa na tatizo la mtaji mdogo na hivyo kushindwa kunufaika na biashara yao.
Alisema kutokana na tatizo hilo, ndio sababu waliomba msaada kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha na Tanzanite One ili wasaidiwe.
Katika hatua nyingine, Kampuni hiyo, imetoa msaada wa mahindi magunia 250 kwa wananchi wakazi wa kata ya Naisinyai ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo kwa jamii inayozunguka migodi yake.
Faisal alisema msaada huo, utasaidia makundi maalum katika jamii na ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kushauri kampuni hiyo, iongeze misaada kwa jamii inayowazunguka.
Kampuni ya Tanzanite One inamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO).
No comments:
Post a Comment