Shirika lisilo la kiserikali la TGNP Mtandao limeendelea na mkakati wa kuwasaidia wakina mama na watoto wa kike wanao ishi katika mazingira hatarishi na wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza na katika warsha iliyofanyika kwenye mtaa wa Msakuzi, kata ya Mbezi jijini Dar es salaam, mwanaharakati ngazi ya jamii TGNP Mtandao, Janeth Biseko alisema suala la unyanysaji wa kijinsia sio kwa wasichana pekee bali hata kwa wanaume pia wamekua wakifanyiwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Alisema mara nyingi matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia inafahamika kutokea kwa wakina mama na wasichana pekee kwani siku hizi imefahamika kuwa hata wakina baba(wanaume) nao hufanyiwa vitendo hivyo.
Vitendo vya ukatili kwa upande wa wakina baba hufanyiwa mara nyingi lakini huwa hawatoi taarifa katika ngazi ya uongozi wa mtaa kwa kuhofia kujidhalilisha,"alisema Janeth. Aliongeza kuwa tunapozungumzia suala la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ni suala la watoto wote bila kujali wakike au wa kiume.
Akizungumza kwenye semina hiyo Mwenyekiti wa mtaa wa Msakuzi, Andrea Evarist Urio alisema wakazi wote wa Mtaa wa Masakuzi sasa muda umefika kusimama na kuanza kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa nguvu moja ili kuweza kutokomoza suala hili katika kata hiyo. Pia alisema vijana wasikae kulalamika bali wanapaswa kuwajibika na endapo watakwama sehemu yoyote wamtafute kwani yeye ndo mwenyekiti wa mtaa huo.
Mwanaharakati ngazi ya jamii mtaa wa Msakuzi, Janeth Biseko akizungumza na wakazi wa mtaa wa Msakuzi waliofika kwenye mafunzo ya kuibua changamoto wanazozipata hasa kwenye ukatili wa kijinsi kwa mtoto wa kike na wakiume uliofanyika katika Mtaa wa Msakuzi kata ya Mbezi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa mtaa wa Msakuzi, Andrea Evarist Urio akitolea ufafanuzi wao kama serikali ya mtaa wanavyojitahidi kupanda na watu wanaosababisha unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa mtoto wa kike wa mtaani hapo kwenye mkutano ulioandaliwa na TGNP Mtandao ili kuibua chngamoto wanazozipata wananchi wa Mtaa huo.
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Msakuzi wakichangia mada kwenye mkutano uliowapa fursa ya kujitambua na hata kujua dhamani yao kwenye mtaa huo hasa kunapotokea unyanyasaji wa kijinsi na njia za kufanya ili kukabiliana na unyanyasaji huo.
Mafunzo yakiendelea kwa wakazi wa Mtaa wa Msakuzi
No comments:
Post a Comment