ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 29, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI

Benki ya KCB Tanzania yadhamini mkutano wa Watanzania wanaoishi nchini Marekani. Mkutano huo utafanyika tarehe 5 – 7 Mei 2017 katika hoteli ya Wyndham Dallas Suites - Park Centrale, Dallas, Texas. Na unategemewa kuhudhuriwa na watanzania elfu moja kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.
Akizungumza kuhusiana na mkutano huu, Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe alisema Texas ni mji wenye watanzania wengi wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara wenye mahitaji ya huduma za kibenki kutoka Tanzania.
“Tunaelewa kuwa shughuli za kutafuta kipato na elimu hupelekea watanzania wengi kuenda sehemu mbali mbali duniani na kuishi huko kwa muda mrefu na hivyo huhitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania.” Alisema Bi. Kombe.

Meneja huyo alisema kuwa Benki ya KCB inawapatia watanzania wanaoishi nje ya nchi huduma bora za kibenki ikiwemo akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi nchini Tanzania. Aliongeza kwamba huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani.
“Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapaswa kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu” alisema Bi. Kombe. Na hivyo tunasema “JIULIZE KWANINI uhangaike kuweka akiba na kuwekeza nyumbani ukiwa mbali na Tanzania wakati benki ya KCB ipo?”
Akamalizia kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo kupitia tovuti ya www.kcbbank.co.tz  na kupata huduma za kibenki wakiwa nje ya nchi.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda.
KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.
Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main naTFA, Mwanza na Morogoro.

No comments: