ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 11, 2017

BUNGENI LEO APRIL 11, 2017

1 comment:

Anonymous said...

Viongozi wa upizani Tanzania ni wanafiki na wasaliti wakubwa kwa watanzania na nchi kwa ujumla. Hivi karibuni kwa macho yangu binafsi kama mara tatu nimekuwa nikisoma katika magazeti ya nje yaliochapisha habari mbaya juu ya Maghufuli na serikali yake na hapana shaka habari hizo mbaya zimetumwa na watanzania na hapana shaka lengo ni kuipaka matope serikali ya Tanzania katika jumuia za kimataifa ili inyimwe misaada au mikopo ya maendeleo. Sasa huko sidhani kama ni kumpaka matope Maghufuli? bali huko ni kuwakomoa watanzania .Ni roho mbaya na upumbavu wa hali ya juu. Nimeangalia katika hiyo clip hapo juu huyo mama wa upizani alivyojaribu hata kuvifitinisha vyombo vya usalama wa nchi. Mtu gani mwenye akili zake kwenye nchi yeyote ile duniani atakaethubutu kusema jeshi la magereza lipewe muhimu zaidi kuliko jeshi la ulinzi wa wananchi? Katika nchi zilizoendelea hata serikali hazihusiki na wafungwa ni biashara za watu binafsi. Kwa mtanzania makini ukiangalia jitihada za upande wa upizani Tanzania utaona kabisa kuwa hawafurahii kuiona Tanzania ikipiga maendeleo wanachoangalia ni maslahi yao ya kisiasa zaidi. Tuseme muheshimiwa raisi ana mwaka mmoja na nusu madarakani na miradi mingi na miundo mbinu ipo katika hatua za kukamilishwa unashangaa mbunge anauliza kwanini kitu fulani hakuna wakati kipo katika ujenzi. Mbunge ana lalamika elimu bure haina ubora? Sasa wakuboresha nani? Wao wabunge katika majimbo yao kazi yao ni nini. Sasa mfano sehemu iliokuwa haina usafiri na yenye usafiri usioridhisha ni sawa? Ni makosa makubwa mtu kama mbunge kubeza kwa dharau na kutia siasa katika masuala ya elimu kwa umma. Pale kwenye elimu bure muheshimiwa raisi ameshatandika msingi na kinachotakiwa ni kuboreshwa kwa mpango mzima wa hiyo elimu bure sio kubeza na kutoa kejeli. Huwezi kuiga siasa za Marekani ukazileta Tanzania. Kama kwa wapinzani kuiga siasa za nje ya nchi hasa Marekani ili kumdisrupt muheshimiwa raisi ashindwe kutekeleza yale muhimu aliyoyaahidi ya maendeleo kwa watanzania katika kipindi chake cha miaka mitano basi hatuna haja ya vyama vingi Tanzania. Raisi wa kwanza wa Zanzibar muheshimiwa Karume alizamiria kwa maneno na vitendo kuiona Zanzibar na wazanzibari ikiwa na maisha sawa kama nchi za ulaya lakini akiwa katika harakati hizo za ujenzi wa nchi baadhi ya wana siasa wakaanza fitna na majungu kuwa hali ya nchi mbaya kimaisha na hawakuishia hapo bali wakatengeza hata mkakati ya kumtoa roho kabisa ili hali ya Zanzibar iwe nzuri, sasa leo Zanzibar iko wapi? Yale mazuri ya karume aliyoyaanzisha imebakia history. Ari na dreams za Maghufli kwa Tanzania hazina tofauti kabisa na hayati karume na nadhani bado watanzania wengi tunajua jinsi sisi watanzania awe wa bara au visiwani tulivyo wanafiki na watu wa kupenda short cut katika maisha lakini kiukweli halisi hakuna short cut katika kutafuta maendeleo lazima kazi na nidhamu na uadilifu wa hali ya juu vizingatiwe ili maendeleo yapaitakane na tulitarajia katika kipindi si kumuona raisi akihaha kujibu habari za kisanii na udaku bali tulitegemea kumuona akijibu hoja ya vipi sisi tunaweza kuidhibiti cargo zote za nchi jirani zikipitipitishwa katika bandari zetu kwani uchumi wa bandari peke yake Tanzania tajiri.