Mbunge viti
maalumu mkoa wa rukwa Bupe
Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili ya kuongezea kununua mifuko ya saruji kwa ajili ya kukarabati shule ya kigonzile
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mbunge viti
maalumu mkoa wa rukwa Bupe
Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameipiga jeki shule ya msingi
Kigonzile iliyopo kata ya Nduli mkoani iringa kwa kuipatia mifuko zaidi ya
ishirini ya saruji kwa lengo la kusaidia ukarabati wa shule hiyo akiwa na lengo
la kumuunga mkono mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati katika juhudi za kuleta
maendeleo ya mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi saruji hiyo Mwakang'ata alisema kuwa ameamua kumuunga
mkono mbunge huyo kwa kuwa ni mpenda maendeleo na mchapa kazi.
“Mimi
napenda kufanya kazi za kimaendeleo hasa za kijamii ndio maana kabati
aliponiambia kuwa anakuja kufanya maendeleo ya ukarabati wa shule ya msingi
kigozile nilikubali haraka kwa kuwa na napenda kufanya maendeleo” alisema Mwakang'ata
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametutuma kufanya kazi kwa wananchi wakawaida
kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi kuliko watu wa kipato cha kati na cha juu
hivyo hata mimi nimeamua kufanya kazi za kwasaidia kuleta maendeleo wananchi
wengi wa chini.
Aidha
Mwakang'ata aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma ili
kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli na
kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko kusubili serikali kuleta
maendeleo.
“Mkiwa
mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi basi nchi hii
itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na wananchi kufanya kazi kwa
nguvu na moyo wa kuinua uchumi” alisema Mwakang'ata
Mwakang'ata
aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo
nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati hivyo nawaomba viongozi
wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa nyingi za kusaidia kukarabati
miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu
bora.
“Hichi
nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma kwenu katika
swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile ambayo ilikuwa
katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake” alisema Mwakang'ata
Mwakang'ata
namkaribisha pia mbunge Ritta kabati kuja Rukwa pia aje asaidie maendeleo kwa
kuwa naye ni mpenda maendeleo na wananchi wa Rukwa wanapenda maendeleo na
ninahakika watampokea kutokana na uchapakazi wake.
No comments:
Post a Comment