Idara Uhamiaji mkoa wa Arusha imewapandisha kizimbani watu watano,akiwamo mchungaji wa kanisa la Pentecostal kwa kosa la kufoji hati ya kusafiria.
Akizungumza na wanahabari leo, Ijumaa, Ofisa uhamiaji mkoa wa Arusha,Ally Dady alisema raia hao wawili wenye asili ya Congo, wakiwa pamoja na mtoto wao, wamebainika kuishi nchini kinyume cha sheria na kujaribu kufoji hati ya kusafiria
Akitaja watuhumiwa wote alisema raia hao wawili Linda Mbaki Diangwe na Glory Mwanza Lubinga walishtakiwa kwa makosa mawili ikiwamo kutoa maelezo yasiyo sahihi ili kufoji hati ya kusafiria.
No comments:
Post a Comment