Advertisements

Friday, April 21, 2017

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MAKUMBUSHO WAPIGWA MSASA KUHUSU ELIMU YA JINSIA

Wanafuzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, wamepata​ mafunzo maalum ya kuwawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika jinsia, yanayowajengea uwezo wa kujitambua vyema na kuisaidia jamii katika maendeleo.
Mratibu wa Uraghibishi wa Wilaya ya Kinondoni chini ya Mtandao wa Jinsia nchini(TGNP) Janeth Mawinza alisema wanatoa mafunzo hayo kupitia klabu maalum za jinsia zilizoanzishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa na kusimamia mambo ya msingi ikiwamo masomo yao.
" Pamoja na mambo ya jinsia ikiwamo kukomesha ukatili wa kujinsia wanafundishwa pia kutambua mahitaji yao muhimu ikiwamo ulinzi na Usalama, mfano katika shule hii kuna zsidi ya wanafunzi 1,400 lakini kuna matundu ya vyoo 10 ambayo matundu mawili ni kwa ajili ya walimu 8 kwa ajili yao hayawatoshi kulingana na idadi yao,"alisema.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Uraghabishi , Bi. Rehema Mwateba akiwasilisha mada kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia kwa watoto wa kike kwa wanafunzi wa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho yaliyofanyika leo jijini Dar leo.(Picha na Geofrey Adroph)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akitoa mafunzo kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makumbusho leo kwenye mafunzo ya Uraghabishi yaliyoaratibiwa na shirika la TGNP Mtandao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho, Bi. Edina Ngelageza akizingumza na wanafunzi pamoja na wageni kutoka kwenye vituo vya taarifa na maarifa vya Jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa club ya jinsia ya shuleni hapo.
Baadhi ya wageni kutoka vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wawezeshaji wakati wa mafunzo ya siku tatu katika shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar leo.
Mraghabishi Mlezi wa Club ya shule ya Msingi Mchangani, Monica Alex  akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa vijana hao ili waje kuwa mabalozi wa masuala ya kijinsia wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya wadau kutoka vituo vya taarifa na maarifa wakichangia mada wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mwezeshaji ambaye ni Mwalimu Mlezi wa Kituo cha  Shule ya Msingi ya Mchangani, Goodluck Busago akitoa mada kwa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Makumbusho wakichangia mada wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa ili kuwaandaa wanafunzi hao ili kuwa mabalozi wazuri wa masuala ya kijinsia katika jamii.

Baadhi ya wanafunzi wa Club ya jinsia katika shule ya Sekondari ya Makumbusho wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule hiyo leo jijini Dar.
Wawezeshaji wa Mafunzo ya Uraghabishi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa club ya jinsi katika shule ya sekondari ya Makumbusho.

No comments: