Advertisements

Friday, April 28, 2017

Ndesamburo amvaa Dk Mwakyembe

Mwanasiasa mkongwe nchini, Philemon Ndesamburo
By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz

Moshi. Moto aliouwasha Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, umemuibua mwanasiasa mkongwe nchini, Philemon Ndesamburo.

Ndesamburo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa mageuzi nchini, alisema Dk Mwakyembe alificha baadhi ya taarifa za sakata hilo ili kuilinda Serikali na mhusika mkuu.

Kauli ya Ndesamburo aliitoa jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu kauli ya Dk Mwakyembe aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, akitaka wanaohoji suala la Richmond walirudishe bungeni.

Bila kumtaja mhusika huyo mkuu, Ndesamburo alisema Dk Mwakyembe ni mtu asiyeeleweka, asiye na msimamo na mwenye ndimi mbili katika suala moja lenye mazingira yanayofanana. “Dk Mwakyembe alisoma ripoti yake bungeni ikiwa na maelezo ya upande mmoja pasipo kumhoji mtu aliyemtaja kama mhusika mkuu wakati anajua vizuri sheria. Natural justice (haki ya asili) inataka umpe nafasi mtu ya kusikilizwa kabla ya kufikia uamuzi, pamoja na kubobea katika sheria, Dk Mwakyembe hakumhoji Edward Lowassa.

Sakata la Richmond liliibuka upya Bungeni wiki iliyopita, baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kumtuhumu Dk Mwakyembe kwa kutomtendea haki Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na alijiuzulu kutokana na sakata hilo.

Habari Zinazohusiana
Lowassa alaza zege bungeni
Richmond yageuzwa mtaji kisiasa
Lowassa atoa msimamo kuhusu Richmond

No comments: