Jumuiya ya waTanzania Rome- Italia Picha kwa hisani ya Tanzania Community Rome- Italy
Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku ya maisha yanayotukabili kila siku ya uhai wetu. Baada ya salamu ningependa kuanza moja kwa moja na swala ya jumuiya za waTanzania nje ya nchi tuipendayo Tanzania, kumekuwepo na migogoro mingi kwenye hizi jumuiya na mishikamano inayoleta umoja kupungua siku hadi siku mpaka inasikitisha na kutia huruma.
Jumuiya za waTanzania ughaibuni zilikua imara sana wakati zilipoanzishwa miaka ya nyuma hasa mwanzoni mwa miaka ya 80 na jumuiya zilikua imara sana wakati huo ikiwemo wanajumuiya wanachama kuwa hai kwa kuchangia michango yao ya kila mwezi hadi mwaka.
Sababu moja wapo kubwa ya jumuiya hizi kuwa hai ni idadi ndogo ya waTanzania iliyokuwepo ughaibuni iliyofanya urahisi wa mawasialino kwa kujuana na kutembelea kama ndugu waliotoka nchi moja tofauti na sasa waTanzania wamekua wengi mpaka wengine imekua vigumu kujuana.
Jumuiya hizi zilianza kugawanyika na kuwa makundi makundi pale viongozi waliochaguliwa kupitisha muda wao na kung'ang'ania kuendelea kuwepo madarakani bila ridhaa ya wanaowaongoza.
Sababu nyingine kubwa na ambayo ndio sababu kuu ni viongozi hawa kutafuna fedha za michango ya jumuiya zao na kutokua wazi na makusanyo ya fedha kutoka kwenye michango mbalimbali ya jumuiya zikiwemo sherehe zilizofanyika kwenye jumuiya hizo zilizohusisha makusanyo ya fedha milangoni au kwa kuuza biadhaa mbalimbali ambazo zimetokana na wanajumuiya wenyewe kuzileta hapo mahali husika, sababu hizi zilikatisha tamaa ya waTanzania ughaibuni kutokuana faida ya kujiunga na jumuiya zao na kuamua kutochangia kwa kuhofia kwa fedha kuliwa kitu kilichosbabisha jumuiya nyingi zishindwe kujiendesha kwa kukosa fadha.
Sababu nyingine ni viongozi wa jumuiya hizi kushindwa kutofautisha faida ya mwanachama hai na asiyekuwa mwanchama hai mfano inapotokea shughuli mwanachama hai atalipa kiingilio sawa na asiyekuwa mwanchama hai, sababu hii inamfanya mTanzania ughaibuni asione umuhimu wa kujiunga na jumuiya.
Sababu nyinginge ambayo ndio inayoonekana kwa wengi ni kuingiliwa na vyama vya siasa kwenye jumuiya za waTanzania ughaibuni. Tangia kufunguliwa kwa matawi ya vyama vya siasa ndani ya jumuiya za waTanzania ughaibuni limeongeza tatizo kubwa la utengano kwenye jumuiya hizo na kuleta matabaka ya itikadi na inapofanyika uchaguzi unageuzwa kuwa wa kisiasa badala kuwa wa kijumuiya, hii imekua sumu kali katika jumuiya za waTanzania ughaibuni. Pamoja na matatizo yaliyokuwepo awali hili la vyama vya siasa wakiwemo viongozi wakubwa wa vyama hivyo kuja ughaibuni kunadi sera na kufungua matawi ya vyama vyao kitu ambacho kimeondoa mshikamano na umoja wa waTanzania ughaibuni ikiwemo wale wasiopenda mambo ya siasa kuondokwa na msisimuko wa kujiunga na jumuiya zao.
Kitu ambacho viongozi wengi wa vyama hizi vya siasa wanachotakiwa kutambua ni kwamba unapokua raia wa nchini ya ughaibuni huruhusiwi kujihusisha na siasa ya vyama nje ya nchi na kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya nchi za ugahaibuni.
Tatizo lingine linaloleta mgawanyiko katika jumuiya zetu ughaibuni ni waTanzania wanakuwa hawapo tayari kuongozwa na waliowachagua wakidhani kuwa viongozi waliowachagua watafanya kazi bila wao huku wakisahau kwamba "JUMUIYA NI WATU SIO VIONGOZI" Viongozi huitwa vingozi kunapokua na watu wa kuwaongoza bila watu hawawezi kuitwa viongozi. Huu mtindo wa kuwachagua viongozi na kuwaacha peke yao ni sababu moja wapo ya anguko za jumuiya za waTanzania ughaibuni na lisiporekebishika hili Jumuiya zote zitakufa.
Sabu nyinini ni viongozi waliokuwepo madarakani kugoma kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya ikiwemo kuwashawishi mpaka wafuasi wao wasitoe ushirikiano kwa viongozi wapya waliochaguliwa, hii inaleta mgawanyiko kwenye jumuiya za waTanzania ughaibuni huu mganwanyiko ni mbaya zaidi na wenye ushawishi mkubwa wa kuuwa jumuiya kwani uongozi ni dhamana kwa watu unaowaongoza na waliokuamimini kukuweka madarakani na muda unapokwisha kubali kuondoka na toa ushirikiano kwa viongozi waliochagulia kuokoa jumuiya yako.
Kitu gani kifanyike kunusuru jumuiya za ughaibuni.
1. Kuondokana na vyama vya siasa.
2. Kuwa wazi kwenye mswala ya fedha.
3. Kukubali kuongozwa na viongozi mliowachagua.
4. Viongozi waliopita na wafuasi wao kuwakubali viongozi wapya waliochaguliwa na kuwapa ushirikiano..
5. kumbuka uongozi wa jumuiya hizi ni wakujitolea leo tupo ya kesho ayajuaye ni mwenyezi Mungu Upendo ni silaha kubwa kwenye Jumuiya zetu kuliko unavyofikiri unapoweka upendo mbele hivyo vitu vinne hapo juu havitakuwepo, siku zote umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, matabaka yawe mwisho tuokoe jumuiya zetu ughaibuni.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu zibariki jumuiya za waTanzania ughaibuni.
10 comments:
Uliyoyasema yote ni kweli kuwa ni vigumu sana kwa WaTanzania kushirikiana. Lakini mimi naona tatizo hapa ni kwamba hatuna 'Upendo.' Upendo umetoweka kuanzia miaka ya 1970. Na mpaka hivi sasa karibu kila mtu anajua lake na huna thamani kama huna pesa. Maana yake "Hapendwi Mtu hapa, Pesa yako tu!" Vijana wengi hivi sasa wamepoteza Upendo na Uzalendo. Pengine vijana wa sasa tusiwalaumu sana kwa kuwa wao wamezaliwa wakati Upendo na Uzalendo umetoweka kwa jamii kubwa. Lakini pia baada ya Upendo na Uzalendo kutoweka, sasa umeingia Udini, Ukabila kidogo, Ukanda, na hivi sasa Uchama, yaani Siasa! Kuna haja ya kufanya jitihada kubwa ili kubadili mawazo ya watu wengi waliyoathilika kutoka jamii ya Uvinu na Uporaji au wizi na kurudi kwenye Uchapakazi, Upendo na Uzalendo. Nikirudi kwenye Jumuiya, bado ipo nafasi kubwa kwa WaTanzania kujiunga na Jumuiya mbali mbali la msingi ni lazima kuwekwa wazi mambo kadhaa yakiwemo: Katiba yenye Mvuto na faida za kuwa mwanachama na matumaini yake. Kingine ni ada ndogo ambayo kila mtu ataimudu, Viongozi thabit, Wazalendo, Wenye Upendo, Waaminifu na Wachapakazi na wenye muda. Pia kuwepo na posho za Viongozi ili wahamasike kuhudumia watu. Watanzani wenye sifa hizi wapo na wanaweza kuhudumia na jumuiya itaenda na itapaa kwenye malengo makubwa.
Mimi naona umbea na wivu umezidi kupundukia aisee.Mimi nakaa hapa Houston aisee nimestukia mtu anayesemwa sana na kuchukiwa ni mtu ambae anamaendeleona mambo Yake super( Mfano mkubwa wa Andrew sanga) .Wivu wakuwaza kumdhuru mtu ,wivu wakumharibia mtu reputation Yake .Kwa kweli nawapongeza sana wake watu ambao wamefanikiwa kutojichanganya na wenzao .Mimi niliambiwa ukifika mamtoni jichanganye aisee najutia.Imagine mtanzania mwenzako anapiga simu Immigration ,FBI,IRS kumshitaki mtanzania mwenzake kweli hawa ni watu wakujichanganya nao?.Kuhama state bei .Kwa kweli Mimi ushauri wangu ni ukija mamtano uwe mwangalifu sana na wabongo aisee.Wabongo tuna wivu sanaaaas.Kutwa kusemana kuzushiana MANENO,kufuatilia NDOA za watu hasahasa wazazi wa watu .
Pole kaka Ibra kwa ajali ya mguu Mungu akubariki.Hii topic muhimu saana rusha comment zote tujadiliane hapa
Ningependa kuongezea kuwa katika hizi jumuia zetu, pamoja na kwamba tupo ughaibuni, lakini bado kuna ukabila wa ndani ambao huwa unaathiri sana ushirikiano kati yetu.
Shukrani Ndugu mwandishi, yaani yote uliyoyaongelea ni point za ukweli kabisa. Mimi ni mkazi wa Washington ,DC tulikuwa na jumuiya nzuri sana ila hizo hizo sababu ulizotoa zimenyong,onyeza raha ya umoja tuliyokuwa nayo. Na tuombeane heri!!
Namshukuru Mungu kwa wachangiaji wote,maelezo yote yapo kwenye jumuiya zetu,shida kubwa kwa pande zetu za Ma ni udini umekuwa shida sana sana,na mwisho umeleta dharau katika jamii zetu kama haupo katika hizo imani zenye watu wengi katika jamii inayotuzunguka. Ukanda umeanza kwa kasi ya kutisha kutokana na mambo ya nyumbani na siasa pia, pia ukiwa na mawazo tofauti ni shida pia,nimeona wengi hawataki kuitwa Watanzania kabisa,pamoja na mambo mazuri na vivutio tulivyo navyo Tanzania,Mungu tusaidie kusimama katika nafasi zetu.
Ndugu hapo juu umetoa point muhimu sana. Mimi nipo nchi ya EU na pia nimeona tatizo hilo. Watanzania tuna hila na roho ya kwanini. Hatupendi mafanikio ya wenzetu. Usemi wa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu hapa hakuna. Unashirikiana na wenzio kwa upendo na kujituma halafu wanaanza kupeleleza familia yako, kochokocho, maneno. Badala ya kuongelea mambo ya maendeleo ya Watanzania, maneno ni juu ya ndugu yako alisema hiki, mbona amesema hivi inakuwa shida kweli kweli. Unagombana na nduguyo kisa Wanaumoja. Mara oo mnafanya shopping kwenye cheap supermarkets. Mbona nguo zenu za bei rahisi. Mambo hovyoo. Watanzania tunamalizana wenyewe kwa wenyewe.
Mtu anaanzisha biashara yake halafu analazimisha umuungishe kwasababu ni mtanzania. Huku biashara ushindani kama unapata huduma hiyo hiyo kwa bei nafuu na kwa eneo karibu zaidi, kwanini uendeshe kilometa hamsini upoteze muda na pesa eti kumuungisha Mtanzania. Basi akishaona umesema hapana huduma yako hailipi kwangu, umekuwa mbaya. Atatafuta kila sababu akusimange na kukuzushia mabaya. Nikweli ukiyajua haya, ukifika nchi za watu unanyamaza kimya. Bora mganda anayekujali kuliko Mtanzania msaka maneno. Mwenzenu nimejifunza maumoja siyataki. nilikuja mwenyewe nitaondoka mwenyewe. Mungu awabariki
Watanzania wa Washington DC nimewanyooshea mikono!
ila watanzania tumezidi majungu hadi kwenye nyumba za ibada!
na siku hizi watanzania tunauana ili kupata mirathi!
Post a Comment