Advertisements

Saturday, May 13, 2017

BreakingNews: MO anataka Simba imlipe Bilioni 1.4


Siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ anataka kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 za Tanzania kutokana na viongozi wa Simba kukiuka makubaliano.

Jana Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu Bw. Evans Aveva, ulisaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
MO anataka kulipwa pesa zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji wa Simba tangu mwaka jana baada ya kubaini kuwa Simba imeingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.

MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.

Simba ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.

No comments: