Mnakaribishwa Sana kushiriki ibada ya Misa kwa lugha ya Kiswahili kama ilivyo desturi
yetu kila mwezi.
Ibada hii pia itajumuisha siku ya kina mama duniani na kwa bahati kubwa sana tutakuwa na mgeni kutoka Tanzania. Baba Askofu Paulo Ruzoka toka Tabora na ataongoza ibada yetu.
Ibada hii itafanyika katika kanisa la Mtakatifu Edward (St Edward Parish)
Anwani: 901 Poplar Grave St.
Baltomire, MD 21216
Simu: 410 362 2000
ZINGATIA MUDA.
Jumapili Tarehe 14 May 2017, muda Ni saa Saba na nusu mchana (1:30).
Ili kuweza kukamilisha ratiba nyinginezo zitakazokuwepo siku hiyo ikiwa ni pamoja na Harambee kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima kule nyumbani Tanzania.
Karibuni sana na tunakuomba usisite kumualika rafiki yako na jirani yako. (palipo na upendo Mungu yupo).
Kwa niaba ya Padri Honest Munishi ni Katibu Tibruss Minja.
No comments:
Post a Comment