Advertisements

Monday, May 15, 2017

KOVA FOUNDATION IKITOA MAFUNZO HOSPITALI MWANANYAMALA


Tarehe 10/05/2017 Taasisi ya Sukos Disaster Management (Kova) Foundation imetoa Mafunzo ya bure kwa Madaktari na Wafanyakazi wengineo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam kuhusu namna ya kukabiliana na Maafa Kama ya moto ikiwa ni pamoja na kufundishwa namna ya kutumia kifaa cha kuzimia moto " Fire Extinguisher" Pamoja na mbinu mbalimbali za kujiokoa iwapo Maafa yakitokea.

Pia wamepata elimu juu ya namna ya kukabiliana na moto utokanao na gesi pamoja na kufundishwa kuhusu matumizi ya kifaa cha kugundua gesi inapovuja "Gas Detector".

Ni Matumaini yetu Elimu Hii itaendelea kutolewa na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi Nchini Tanzania.

No comments: