Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema alikasirika sana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa 2015.
Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, 2015 akidai kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi na miezi miwili baadaye aliitangaza Machi 20, 2016 kuwa terehe mpya ya kupiga kura.
Hatahivyo, CUF ilisusia uchaguzi huo wa marudio ambao Dk Ali Mohamed Shein alishinda kiti hicho kwa kishindo.
Uchaguzi huo ulifutwa siku ambayo mshindi wa kiti cha urais alitakiwa atangazwe huku matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa na kura za majimbo tisa zikiwa zimeshahesabiwa pia nafasi za uwakilishi na udiwani zilishatangazwa na kutolewa hati za ushindi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu baada ya kutembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) wanaochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Maalim Seif amesema, “Kama binadamu nilikasirika baada ya Jecha kufuta matokeo yale. Lakini mimi ni mtu mzima niliweza kujidhibiti mwenyewe hisia zangu, pia niliweza kutoa wito kwa watu kuwa wavumilivu, lakini kiukweli nilikasirika sana.”
Amesema kitendo cha Jecha cha kutangaza matokeo aliita cha kihuni kwa sababu ukishakubali mfumo wa vyama vingi ambao unawapa nafasi wananchi kufanya uamuzi kuhusu Serikali wanayoihitaji iwaongoze, lazima ukubali na matokeo
No comments:
Post a Comment