Advertisements

Saturday, May 13, 2017

MAKUNYANYO YA BILIONI 76 WIZARA YA ARDHI YAVUNJA REKODI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Yamungu Kayandabila

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imefanikiwa kukusanya Sh76bilioni cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.

Akiongea katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Yamungu Kayandabila amesema kiwango cha makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufikiwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Wizara imekusanya Sh76 bilioni cha kodi ya pango la ardhi.

“Juhudi za kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa zinaendelea vizuri licha ya changamoto iliyopo hususan mwamko wa wananchi katika kulipa kodi.” amesema Dkt. Kayandabila.

No comments: