Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro leo (jana), kulia ni Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine Mungu.
Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine Mungu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro leo.
Afisa Uhusuano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi mkoani morogoro leo.
Bw. Fabian Felician akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliofanika mkoani Morogoro leo.
Afisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Bw. Simbo Swai akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanyika mkoani Morogoro leo.
Bi. Hilda Msemo kutoka Mzinga Corporation akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanika mkoani Morogoro leo.
Baadhi ya
washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na
mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt.
Francis Michael mkoani Morogoro leo.
Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini
katika mikoa minne, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri
kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya
waajiriwa wao.
Akizungumza
katika semina hiyo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko Dkt. Francis Michael .
Amesema
kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea
katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo
hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.
“Ni muda
muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua
madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Dkt. Michael.
Katika hotuba
yake, Dkt. Michael alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi
wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga
wakiwa kazini.
Mfuko wa
Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na
umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura
ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
Dkt. Michael
amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa
waajiri kwa kutambua kuwa waajiri ndio
wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini
pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
Akitoa mada
juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo,
Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa
wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Naye
Mwanasheria Mwandamizi wa Mfuko huo Bi.Irene Mungure amesema, ni muda mwafaka
kwa waajiri kutambua wajibu wao katika mfuko ikiwa ni pamoja na kutambua
madhara ya kutokutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria.
Katika
uzinduzi wa semina hizo jana Makao Makuu ya Nchi Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Emmanuel Humba,
alifafanua zaidi juu ya haja ya waajiri kuufahamu vizuri Mfuko namna
unavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia,
kuugua ama kufariki. Aidha, alisema kuwa waajiri ni wadau wakuu wa uendelezaji
Mfuko.
Bw. Humba
aliwaasa waajiri kutokufanya udanganyifu na ubadhilifu hasa katika
uwasilishwaji wa michango kwani itakuwa ni kuudidimiza Mfuko na ni kosa
kisheria na waajiri watakaojihusisha watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu
wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi
Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015
Semina hiyo imefanyika
katika mikoa ya Dodoma,Kilimanjaro, Morogoro na Arusha.
No comments:
Post a Comment