Advertisements

Thursday, May 18, 2017

Mtoto Doreen aingia kwenye upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo Marekani

Mwanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent, Doreen Mshana akiwa wodini akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mercy iliyopo jijini Sioux.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi; mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Marekani. Mtoto Doreen Mshana, ameingia kwenye chumba cha upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo asubuhi hii nchini Marekani anakotibiwa huku madaktari wakiwataka Watanzania wamuombee.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu(CCM) ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa madaktari wanaingia kwenye chumba cha upasuaji huo asubuhi hii.

Upasuaji huo unatajwa kuwa ni mkubwa na mgumu.

“Taifa na kila mtu tumuombee mtoto wa Doreen. Anaenda kufanyiwa upasuaji mgumu wa uti wa mgongo.” umesema ujumbe wa madaktari hao aliotumiwa Nyalandu.

No comments: