Advertisements

Friday, May 12, 2017

TADB, TAHA WAPANGA KUSAIDIA SEKTA YA MALI MBICHI NA MATUNDA (HORTICULTURE)


Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) wakati wawili hao walipokutana kujadiliana juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.


Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kushoto) akihimiza jambo juu ya umuhimu wa sekta ya malimbichi na matunda katika uchumi wa Tanzania kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (hayupo pichani) wakati wawili hao walipokutana kujadiliana juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha. Kulia ni Meneja Mkuu wa Maendeleo wa TAHA, Anthony Chamanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kulia) akimuelezea Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (hayupo pichani) nafasi ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Chacha.
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi akieleza utayari wa TAHA wa kushirikiana na TADB katika kukwamua changamoto zinazoikabili sekta ya malimbichi na matunda nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) nafasi ya TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya TADB na TAHA katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) mara baada ya mkutano wao unaolenga kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arush

Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA) zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza tija kwa kilimo hicho.

Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na kilimo kwa ujumla nchini.

“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

No comments: