Advertisements

Saturday, May 13, 2017

TADB YAFUNGULIWA MILANGO MANYARA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (katikati) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri.
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri (kulia) akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (katikati).

Na mwandishi wetu, Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwenda kuwekeza mkoani humo kwa kuwapatia kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mkoa huo.

Akizungumza wakati wa mazungumzo na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake, Mhe. Bendera amesema mkoa wa Manyara una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo kulinganisha na mikoa mingini nchini.

“Mkoa wa Manyara una fursa nyingi sana ambazo Benki inaweza kutoa mikopo ambayo nina uhakika itarudishwa kwa wakati kwa sababu watu wa Manyara ni waaminifu sana,” alisema Mhe. Bendera.

Akizungumza na Mhe. Bendera, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta za kilimo na mifugo ni sekta za kipaumbele ambazo zinazopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.

Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza tija sekta hizo.

“Benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” aliongeza. TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akitambulisha mikopo na huduma zinazotolewa na Benki yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (kulia).
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri (kulia) akizungumzia hali ya ushirika mkoani Manyara wakati wa ugeni wa TADB walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (katikati) akizungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo na mifugo zinazopatikana mkoani Manyara wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera akisisitiza umuhimu wa TADB kwa mkoa wa Manyara.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera wakati akisisitiza umuhimu wa TADB kuwekeza mkoani Manyara.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akisisitiza utayari wa Benki yake kuwekeza mkoani Manyara.

No comments: