Advertisements

Wednesday, May 10, 2017

Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI

Washington, Marekani. Rais Donald Trump amemfuta kazi Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi (FBI), James Comey kutokana na namna alivyoshughulikia barua pepe za aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton.

Hata hivyo, wanachama wa Democratic wamesema kuwa Comey alifukuzwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa inachunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kwamba Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa Bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump alimwandikia barua Comey kumwambia kuwa alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Sessions alisema kuwa Wizara ya Sheria ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu wa sheria na mwanzo mpya unahitajika.

Ikulu ya Whitehouse imesema mrithi wake atapatikana haraka.

Pamoja na hayo yote, kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Chuck Schumer amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.

No comments: