Advertisements

Tuesday, May 9, 2017

Wateule wa Chadema ubunge wa Afrika Mashariki waanza kampeni


By Reginald Miruko, Mwananchi

Dodoma. Wagombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chadema wapo katika viwanja vya Bunge wakipiga kampeni kabla ya uchaguzi utakaofanyika kesho.

Walioanza kuonekana tangu jana jioni ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekia Wenje na Waziri wa zamani, Lawrence Masha.

Wagombea wengine waliopitishwa na Kamati Kuu ya Chadema kuwania nafasi hiyo ni Josephine Lemoyan na Pamela Massay.

Masha na Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4 ambao Chadema ilipeleka majina yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na kuhitimishwa kwa wao kupigiwa kura za Hapana.

Katika uchaguzi wa awali, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa Eala.

Kwa upande wa CCM, walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na kutoka CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo.

No comments: