Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Patrick Kipangula na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) akiongea wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Patrick Kipangula.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea jezi kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) mara baada ya kikao na uongozi huo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa michora ya ramani za viwanja vya michezo vinavyotarajiwa kujengwa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) leo Jijini dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na uongozi wa uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo Jijini
Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM)
Na
Lorietha Laurence
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Klabu ya michezo ya
Afrika Lyon kwa kutumia mchezo wa mpira
wa miguu kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa tembo.
Waziri
Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na
uongozi wa klabu hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari MAELEZO.
Katika
kikao hicho uongozi wa timu hiyo ulimueleza Waziri kuwa timu yao imeamua
kushiriki vita dhidi ya vitendo vya mauaji ya tembo kwa kuandika ujumbe maalum
katika jezi za timu hiyo kuelimisha jamii dhidi ya vitendo hivyo.
“ni
jambo zuri kuhakikisha jamii inapata burudani ya mpira wakati huo huo inaelimika
kupitia ujumbe unatolewa na wachezaji katika jezi zao”Dkt Mwakyembe alisema.
Kwa
hivyo, aliushukuru uongozi wa timu hiyo kwa juhudi zao hizo na kukieleza
kitendo hicho kuwa ni “cha mfano na kujivunia”.
Aliongeza
kuwa Serikali inajivunia na kuthamini mchango wa wananchi wazalendo
wanaojitolea kujenga taifa na kulinda rasilimali zake kama timu ilivyofanya
timu hiyo.
Aidha
Waziri Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa ni
jambo jema linalofanywa na klabu hiyo katika kuhakikisha inakuza
na kuendeleza vipaji kwa vijana mbalimbali nchini jambo ambalo
linasaidia kuinua sekta ya michezo.
Pia
aliwapongeza kwa kupata fursa ya kutembelea nchi ya China kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu michezo na kuwataka kuitumia fursa hiyo ipasavyo
kwa kujifunza kwa bidii ili watakaporejea waweze kufundisha vijana wengine wa kitanzania.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Afrika Lyon Bw. Rajuu Kangezi ameeleza kuwa mkakati
wa klabu hiyo ni kuhakikisha kuwa inajenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa
matumizi ya jamii ili kuendeleza michezo nchini hivyo ameomba ushirikiano na serikali katika
kufanikisha mikakati hiyo.
“Tuna
mipango mingi ya kuhakikisha tunakuwa na viwanja vizuri vya michezo na hili
haliwezi kufanikiwa bila kuishirikisha serikali na viongozi wake hivyo tunaomba
ushirikiano wa serikali katika kuhakikisha tunafanikisha jambo hili”
Katika
kikao hicho uongozi wa klabu hiyo ulimkabidhi Waziri Mwakyembe jezi namba tano
“5” ya klabu hiyo kwa ajili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment