Advertisements

Friday, May 26, 2017

WIZARA YA VIWANDA YAANZISHA DAWATI LA BIASHARA.


Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha dawati la wepesi wa kufanya biashara ambao lina jukumu la kuondoa ugumu wa kuanzisha na kuendesha biashara  nchini.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni Mhe. Jamal Kassim Ali.

“Ujenzi wa Viwanda nchini unategemea zaidi mazingira ya uwekezaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi yenye miundombinu wezeshi,sera mbalimbali,mifumo ya kodi na mifumo ya upatikanaji wa vibali  vinavyotakiwa kisheria ambayo ni majukumu ya Serikali”Alisema Mhe.Mwijage.


Aidha Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji imeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wa kitanzania ili kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

Miongoni mwa Mikakati hiyo ni Mafunzo yanayotolewa kwa watanzania wenye nia ya kuwekeza katika viwanda juu ya kuibua mawazo ya kibiashara,kuanzisha ,kuendesha na kusimamia biashara kupitia SIDO,kutoa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuchagua teknolojia sahihi inayoendana na wazo la ujenzi wa kiwanda alilonalo Mtanzania kupitia TIRDO,TEMDO na CAMARTEC na namna ya kupata ama kukuza mtaji wa ujenzi wa viwanda kupitia NEDF,SIDO na TIB.

Pamoja na hayo Wizara imeandaa mwongozo kwa Mikoa,Wilaya,Kata na Vijiji kutenga maeneo ,kusimamia sheria,kanuni,taratibu na kutoa maelekezo kwa wawekezaji.
“Watanzania wnaaotaka ama walio na mitaji mikubwa wanaweza kuwekeza kupitia maeneo ya EPZA ambayo yametengwa mahsusi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi,Pia wanaweza kuwasiliana na TIC kupata vivutio mbalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji,Alisisitiza Mhe.Mwijage.

No comments: