Advertisements

Thursday, June 1, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA INAFANYA ZIARA KATIKA MIJI MIKUU NCHINI MAREKANI

Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi, Dismas Assenga.
Raisi wa Jumuiya ya watanzania waishio Houston Marekani Bw. Daudi Mayocha (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mijini Houston.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (aliesimama, wapili kushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki ya KCB kwa baadhi ya watanzania (pichani) wanaoishi katika mji wa Houston.
Raisi wa jumuiya ya watanzania waishio Dallas Marekani Bw. Ben Kazora (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mjini Dallas.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas.

Benki ya KCB Tanzania kupitia dawati lake la Diaspora Banking inafanya ziara katika miji waishio watanzania nchini Marekani. Ziara hii imeanza tarehe 26 Mei na kutegemewa kumalizika tarehe 7 Juni. Miji inayotembelewa ni Washington Dc, Houston, Tx, Dallas, Durham Raleigh, Nc Boston, Ohio, Minnesota Na Chicago.

Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe akizungumza kuhusiana na ziara hii, alisema “Kuna watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi na wanahitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania, hivyo Benki ya KCB inatembelea miji ya Marekani yenye watanzania wengi ili kuwapatia huduma bora kwa haraka, usalama na bila usumbufu”.

Huduma za kibenki wanazopatiwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni; akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi nchini Tanzania.

“Huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani” alisema Bi. Kombe.

Akizungumza na Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Kombe na watanzania wanaofanya kazi ubalozini, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Dismas Assenga alifuraia ujio wa benki ya KCB nchini Marekani. “Watanzania wanaoishi Marekani wanahitaji sana kuwekeza nyumbani hivyo tutafurahi mkifikia watanzania wote kutoka miji tofauti ya Marekani” alisema Kaimu Balozi.

Bi. Kombe alimaliza kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo, mteja anahitaji kua na nakala ya Pasi ya kusafiria, Leseni ya udereva au risiti ya huduma za umeme au maji (utility bills).

Vile vile wanaweza kutuandikia kupitia barua pepe diasporabankingtz@tz.kcbbankgroup.com na kupata huduma za kibenki wakiwa nje ya nchi.

Jiulize kwanini uhangaike kupata huduma za kibenki Ughaibuni?

Kuhusu Benki ya KCB


Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda.

KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main naTFA, Mwanza na Morogoro.
No comments: