ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 23, 2017

EXCLUSIVE: BEN POL KAKUBALI KUMUOA EBITOKE NA KUISHI NAYE MILELE.


Mwana RnB Ben Pol akiwa katika picha ya mahaba na mchekeshaji Ebitoke

Hatimaye Ben Pol na Ebitoke wakutana Live! Ni baada ya mwanadada huyo wa kwenye tasnia ya uchekeshaji hivi karibuni kufunguka kwamba mwanaume anayemzimia sana kuliko wote ni mkali wa miondoko ya RnB nchini, Bernard Paul, almaarufu kwa jina la Ben Pol. Watu wengi kupitia mitandao ya kijamii walijitokeza kutoa maoni yao kuhusu kauli ya mwanadada huyo.
Ben Pol na Ebitoke katika pozi moja matata sana, kama vile ‘Wedding Portrait”
…sogea karibu yangu nikukumbatie Beni!

Wengi walimponda kwa kumwambia aache kujipendekeza na kutafuta kiki ili ajulikane na mwanamuziki huyo na wale ma-opportunist a.k.a wazee wa ganda la ndizi kuteleza wakaamua hata kufungua akaunti za instagram kujaribu kupata followers wengi kupitia kastori hako. 

Pamoja na maneno lukuki toka kwa mashabiki na mabingwa wa chuki binafsi (haters) wawili hao wamekutana na kula bata kiaina kisha kupiga photo shoot. Picha hizo zimelipua upya wafatiliaji wa mitandao ya kijamii hasa baada ya kila mmoja kuweka kwenye akaunti yake na kuandika ya moyoni mwake.
……..mm ndiye Mrs Ben Pol jamani
Katika kursa zao za Instagram, Ben Pol na Ebitoke wameandika:
“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika? Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, na labda huyo Mtu kesho hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako . Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST !!@ebitoke #blessed “
Mwanadada Ebitoke safari hii amekuwa na machache kuelezea hisia zake kwa kuandika:
“Asante Mungu
You are the real GENTLEMAN
@iambenpol

No comments: