Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kulia)
akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya
Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera Jeremiah (kushoto) Ripoti ya Uchaguzi
Mkuu wa Tanzania wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015 wakati Kamati hiyo ilipotembelea
Ofisi za Tume leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (katikati) akitoa ufafanuzi
kuhusu majukumu ya Tume kwa Wabunge wa
Bunge la Msumbiji ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa waliotembelea Ofisi za NEC jijini Dar es salaam kujifunza
namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba. Kushoto ni Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mhe. Lucas Chomera Jeremiah na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa NEC Bw. Hamis Mkunga.
Mkurugenzi wa Huduma za
Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto)
akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge
la Msumbiji namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inavyotekeleza majukumu
yake kwa mujibu wa Katiba.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera
Jeremiah (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Msumbiji na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania leo jijini Dar es salaam, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la
Msumbiji wamezitembelea Ofisi za NEC kwa lengo la kujifunza na kubadilishana
uzoefu katika masuala ya Uchaguzi.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia)
akisalimiana na Wabunge wa Bunge la Msumbiji na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Utawala na Serikali za Mitaa wa nchi hiyo waliotembelea Ofisi za NEC kujifunza
na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa chaguzi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment