Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO ya
siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,
(WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali
kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki
kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo
hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya
Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23,
2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na
binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo
mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki
Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza
kwenye ufungaji wa mafunzo hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha
Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko
kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika
kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa
kazini.
Dkt.Benjamin Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa jopo la wataalamu walioendesha mafunzo hayo, Dkt.Robert Mhina kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Arnold Mtenga
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Aida O. Salim
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Alex Shuli
Dkt. Machumani Kiwanga akisikilzia kwa makini hotuba ya ufungaji
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akifuatilia kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya.
Washiriki wakisikiliza hotuba
Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu, WCF akiwa na Daktari bingwa wa upasuaji na majeruhi kutoka tasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina, ambaye ndiye alijkuwa mwenyekiti wa jopo la wataalamu waliotoa mafunzo hayo
No comments:
Post a Comment