Advertisements

Friday, June 2, 2017

MSHINDI KOMBE LA SPORTPESA KUWAVAA EVERTON DAR JULAI 13

Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (kushoto) akimfurahia na kumpigia makofi,kijana Abubakar Said wa Kituo cha michezo cha Wakati ujao wakati wa Kliniki iliyofanyika Uwanja wa Taifa, leo. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa pili kushoto) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone (kushoto) Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, wakati wakiwasili Uwanja wa Taifa leo Juni 1, 2017 kwa ajili ya kukagua timu za vijana (Academy) wakati wa zoezi la kuhamasisha vijana katika mchezo wa mpira wa miguu, lililoongozwa na mchezaji huyo wa zamani wa Everton.
Mtoto Hamis Kassim wa Kituo cha michezo cha Bom Bom, akionyesha umahiri wake wa kuchezea mpira wakati wa hafla hiyo ya Kliniki iliyoongozwa na mchezaji wa zamani wa timu ya Everton. Leon Osman.
Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone,akizungumza na waandishi wa habari.


Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

KAMPUNI ya SportPesa imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa Uingereza, Everton. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.

Tangazo hilo limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Mkuu wa masoko wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi wa Everton Fc ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na wanahabari. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman,akichezea mpira na vijana.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Lenox Musombo, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone. 
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Zuberi Ada, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. 
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Wakati Ujao Duce, Ezekiel Msuva ambaye ni mdogo wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania,Simon Msuva, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa Nne kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Montage Ltd, Teddy Mapunda, wakipita kukagua timu za vijana za Academy, wakati wa Kliniki ya kuwahamasisha katika mchezo wa Soka katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone, wakati wa hafla hiyoiliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,leo.

SportPesa ilitangaza Mei 24 kwamba michuano ya SportPesa Super Cup itafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikishirikisha timu nne (4) za Tanzania dhidi ya timu nne (4) kutoka Kenya. Timu sita (6) kati yazitakazoshiriki michuano hiyo ni klabu washirika rasmi wa SportPesa. Simba SC, Young Africans SC na Singida United FC ni washirika wa SportPesa Tanzania wakati Nakuru All Stars, AFC Leopards na Gor Mahia ni washirika wa SportPesa kutoka Kenya. Tusker FC ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa ya Kenya wakati Jang’ombe Boys FC ni vinara katika Ligi Kuu ya Zanzibar.
Akifurahia ujuio wa Everton, Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov alisema; “Tuna furaha kuwakaribisha Everton nchini Tanzania, kwani ziara yao itakuwa na manufaa siyo tu kwa klabu za hapa zitakazopata fursa ya kucheza na mabingwa hao mara 9 wa Ligi Kuu ya England, bali pia na taifa zima kwa ujumla. 

“Katika ziara hiyo tutashirikiana kufanya shughuli kadhaa za kurudisha kwa jamii. 

“Tanzania inapaswa kujiandaa kupata uzoefu mkubwa kutokana na uwepo wa Everton mjini hapa.” 

Robert Elstone, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton alisema: “Maandaizi ya mwanzo wa msimu mpya ni kipindi muhimu sana kwetu kwani kwa kocha Ronald Koeman na benchi lake la ufundi wakiwaandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mkubwa ujao. Kuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kuja kucheza Tanzania itakuwa ni sehemu muhimu ya maandalizi hayo.

“Tunafungua milango mipya na hatuna shaka kwamba tutapata marafiki na kuongeza mashabiki wetu kkmataifa tutakapokuja Julai.

“Najua Ronald Koeman na wachezaji wanajiandaa kuja kucheza mechi nzuri dhidi ya moja ya klabu bora ya Afrika Mashariki.”
SportPesa tangu ilipozinduliwa Tanzania Mei 9, 2017, imethibitisha nia yake ya kufanya mapinduzi ya soka nchini hapa kwa kuzidhamini klabu tatu za soka, ikichangia Sh. Milioni 50 za Kitanzania katika kuisapoti timu ya taifa ya vijana ya U-17 Serengeti Boys ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya AFCON ya vijana nchini Gabon, imetangaza michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inaweza kuwakutanisha miamba wa soka wa Tanzania, Yanga na Simba katika nusu-fainali au fainali, na pia kumshuhudia bingwa wa Kombe la SportPesa akiwavaa miamba hao wa Uingereza.

No comments: