Advertisements

Friday, June 2, 2017

NHC TANGA YAWATANGAZIA KIAMA WANAOGUSHI FOMU ZA UPANGISHAJI

Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga na Fundi Mchundo wa Shirika hilo jana wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea 
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati 
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani
Tanga Mussa Kamendu kulia akionyeshwa moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga na Fundi Mchundo wa Shirika hilo wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea 
Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua ukarabati wa nyumba za shirika hilo ambazo zinafanyiwa marekebisho
Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana 
Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kupitisha mfumo wa maji taka 


SHIRIKA la Nyumba la Taifa Mkoani Tanga (NHC) limewa tahadharisha watu wanaoghushi fomu za maombi ya kupangisha katika nyumba zao na kuziuza kwa wananchi kuacha mara moja tabia hiyo kwani watakabanika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Shirika hilo,Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mipango mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuzifanyia ukarabati nyumba wanazozimiliki ili ziweze kuwa katika muonekana mzuri kwa zile ambazo zimeonekana kuchakaa.
Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kughusi fomu ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa kuzisambaza kwa wengine na kuwauzia jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliopo.
“Ukiangalia sisi kama shirika tumekuwa tukitoa fomu kwa wananchi ambao wanataka kupangisha kwenye nyumba zetu lakini katika hilo kumejitokeza baadhi ya watu wanazitoa kopi na kuziuza kitendo ambacho ni uvunjifu wa taratibu tulizoziweka “Alisema.
“Jambo hili ni hatari hasa kwa ustawi wa shirika letu kwani
linachangia kukosesha mapato hivyo tutahakikisha tunawa shughulikia watakaobainika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi yake kwa maslahi ya ustawi wa shirika letu “Alisema Meneja huyo.
Aidha alisema licha ya jitihada hizo lakini pia wameweka mpango
kabambe wa kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa madeni yao ya pango kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa shirika hilo kuweza kujiendesha na kuweza kufanikisha mipango ya maendeleo.
Kamendu aliwataka pia wapangaji wao wazingatie mikataba walioingia na shirika hilo ikiwa pamoja na utunzaji mazingira ya nyumba hizo na kulipa kodi kwa wakati kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa.
Aidha pia alisema hivi sasa tayari shirika hilo limekwisha anza
kufanya ukarabati wa nyumba hizo ikiwa pamoja na kuboresha mifumo ya maji taka, kuweka bati mpya na upakaji wa rangi katika nyumba zilizopo katika maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Tanga.
Alisema miongoni mwa nyumba walizoanza kuzifanyia ukarabati ni pamoja na zilizopo maeneo ya Chumbageni,kwa karatunga,barabara 4,6,Bombo na Raskazoni ambapo marekebisho hayo yanafanyika kwa lengo la kurudisha ubora wa nyumba hizo.
Aliongeza kuwa marekebisho yanayofanywa na shirika hilo yana lengo la kuhakikisha nyuma zao zinakuwa katika ubora mzuri ambao utamfanya mpangaji aweze kuishi kila kukumbana na usumbufu wa aina yeyote.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments: