Advertisements

Wednesday, June 21, 2017

PRESS RELEASE KARIBU MUSIC CENTER

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

21, JUNI 2017
Zaidi ya vijana 20 wenye vipaji vya muziki wanatarajiwa kupata mafunzo ya bure ya kukuza vipaji vyao katika uimbaji, upigaji wa ala na utayarishaji wa muziki na nyongefu katika muhula utakaoanza Mwezi Agosti mwaka huu katika kituo kipya cha muziki kinachojulikana kwa jina la Karibu Music Centre.

Kwa mujibu wa msemaji wa kituo hicho, Bw Richard Lupia, katika muhula huu unaoanza mwaka huu, wanafunziwatapatikana baada ya usaili utakaofanyika Jumamosi ya Juni 24 mwaka huu kuanzia saa nne asubuhi na kuendelea.

“Lengo ni kupanua wigo wa Sanaa na kukuza soko la ajira ambapo siku za karibuni, vijana wameonekana kujiajiri kwa kiasi kikubwa kwenye Sanaa, lakini kuna mahala wanakwama, na tumegundua kwamba wanakwamakwenye utaalamu wa jinsi ya kuifanya Sanaa kuwa biashara, alifafanua Bw Lupia.

Amesema uhitaji wa elimu ya Sanaa ni mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya vyuo na taasisi vya kuikuza sanaa hiyo vilivyopo nchini. Hali hiyo inasababisha wasanii wengi kuibuka na kupotea kwa sababu ya kutokuwa nautaalamuwa kazi wanazofanya.

Karibu Music Centre ina lengo la kuzalisha wasanii wa kimataifa watakaopiga muziki wenye asilimia kubwa ya uasilia utakaotambulisha Sanaa ya Tanzania nje ya mipaka  ya nchi.

Kutakuwa na waalimu wa aina nne, wa uimbaji, Upigaji wa ala za muziki, utayaishaji wa muziki na utayaishaji wa picha nyongefu(Video).

Karibu Music Centre kwa mwaka huu inaanza na wasanii wa Dar es Salaam peke yake na mikoa ya karibu ambapo mwakani utaratibu wa wasanii kutoka mikoani huenda ukatangazwa kutegemea na mwamko wa wafadhili, ingawa Karibu itaendelea kutoa taaluma hiyo bure.
No comments: