Rais John Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wakiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu baada ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya nchini Canada, Profesa John Thornton.
Barrick Gold Corporation ni kampuni mama ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia.
“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike,” amesema Rais.
Ameonya viongozi hao kuhusishwa katika taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia).
No comments:
Post a Comment