Viongozi na walimu wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakishangilia baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujitambua na ujasiri katika kambi iliyofanyika hivi karibuni eneo la Mombasa, Dar es Salaam. Zaidi ya 36 kutoka mikoa mbalimbali walishiriki kwenye mafunzo hayo. Pia katika mafunmzo hayo yaliyofanyika kwa wiki moja yalihudhuriwa na viongozi kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar
Mgeni rasmi katika hafla ya kufungakambi hiyo yalifanywa na Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba, ambaye aliwaasa kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwenda kuanzisha kambi za kuwafundisha wanachama mikoani wanakotoka. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akimkabidhi cheti mmoja wa walimu waliohitimu mafunzo hayo.
Grace Shaba akimkabidhi m cheti mmoja wa wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Jestina Philip
Grace Shaba akimkabidhi cheti Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Sharifa
Grace Shaba akimkabidhi cheti Happy wa Makao Makuu ya TGGA Dar es Salaam
Mwalimu wa Girl Guides , Valentina akikabidhiwa cheti
Kiongozi wa Girl Guides wa TGGA, Makao Makuu, Rehema Kijazi akipokea cheti kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Grace Shsba. Katikati ni Kamishna Rose.
Michelle kutoka Rwanda akifurahi baada ya kukabidhiwa cheti
Kiongozi wa Girl Guides kutoka Madagascar akipokea cheti
Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi, akipokea cheti
Kiongozi kutoka Tanga, akipokea cheti
Twarhiya Hussein kutoka Lindi mtoto pekee aliyehitimu mafunzo hayo na kufanya vizuri, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba.
Rachel Baganyila kutoka Uganda akifurahi kupokea cheti
Ni wakati wa kucheza ngoma
No comments:
Post a Comment