Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Match Industries Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) wamejitoa kusaidia maisha ya mamia ya Watanzania kwa kujitolea damu ambazo zitatumika katika hospitali mbalimbali nchini.
Katika tukio hilo la kujitolea damu ambalo lilifanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, wafanyakazi 40 walijitolea damu zao ambazo zitapelekwa kusaidia wagonjwa katika hospitalini zenye uhitaji mkubwa wa damu.
Akizungumzia umuhimu wa kutoa damu, Meneja Msaidizi wa Hospitali ya Sanitas, Dr. Sajjad Fazel alisema utoaji wa damu huo ni muhimu kwa kusaidia maisha ya watu wengine kwani hata chupa moja ya damu ina muhimu mkubwa na inaweza kusaidia kuoa maisha ya watu watatu.
“Kuna uhaba wa damu, kwa kila Mtanzania ahakikishe kuwa anaonyesha uzalendo na upendo wako kwa Watanzania wenzake kwa kuchangia damu na kuokoa maisha yao,” alisema Dk. Fazel.
Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Match Industries Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) wakijitolea damu.
No comments:
Post a Comment