Advertisements

Tuesday, July 11, 2017

BALOZI MLIMA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WA INDIA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Neena Malhotra. Wawili hao walizungumzia namna nchi zao zinatakavyoweza kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali kama za uwekezaji, miundombinu, afya, elimu, TEHAMA, biashara na kilimo. Aidha, Balozi Mlima alimuomba asaidie kuhamasisha wawekezaji kutoka India kuja kuwekeza nchini katika viwanda ili kuunga mkono agenda ya Serikali ya awamu ya tano inayoweka mkazo kwenye viwanda.

Ujumbe wa Tanzania (kulia) na ule wa India ukiongozwa na Makatibu Wakuu wao ukiwa katika majadiliano ya namna ya kuboresha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na India ambayo yemedumu kwa miaka mingi sasa

Balozi Mlina akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu wa India


picha ya pamoja

No comments: