Advertisements

Wednesday, July 19, 2017

Jaji Upendo Msuya afariki dunia

By Hussein Issa, Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa mudamrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga

Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

No comments: